Wednesday, May 9, 2012

Simba waenda sudan na 19


Mabingwa wa Tanzania Simba SC imeondoka leo mchana kuelekea Sudan na shirika la ndege la Kenya Airways. Msafara wa Simba una wachezaji 19 na viongozi saba.

Wachezaji wanaoondoka ni Juma Kaseja, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Derick Walulya, Amir Maftah, Juma Jabu.

Wengine ni Obadia Mungusa, Kelvin Yondani, Victor Costa, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Patrick Mafisango, Haruna Moshi, Machaku Salum na Uhuru Selemani, Felix Mumba Sunzu, Emmanuel Arnold Okwi, Edward Christopher Shija na Gervais Arnold Kago.

Viongozi wanaofuatana na timu hiyo ni Ismail Aden Rage (MB), Swedy Fikirini Mkwabi, Milovan Cirkovic, Amatre Richard, James Stephan Kisaka, Dk. Cosmas Kapinga, Nicholaus Menrad Nyagawa na Ezekiel Kamwaga.

Mkuu wa msafara huo ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Hussein Mwamba.

Wachezaji wawili; Nassor Said Masoud (Chollo) na Juma Said Nyoso hawajakwenda Sudan kwa vile wanatumikia adhabu zao za kukosa mechi kutokana na kuwa na kadi.

Mechi ya Shandi na Simba itapigwa Jumapili ijayo katika Uwanja wa Shandi wenye uwezo wa kuchukua washabiki 10,000. Mji wa Shandi uko Kaskazini Magharibi mwa Sudan na uko umbali wa kilomita 150 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Source; aboodmsuni.blogspot.com

No comments:

Post a Comment