Wednesday, May 2, 2012

YAMETIMIA SIMBA BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA 2011/2012
1.TANZANIA BARA
   Timu za Simba leo jioni imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara baada ya wapinzani wao waliokuwa wakiwafuatia kwa karibu Azam kupoteza mchezo wao wa leo dhidi ya Mtibwa sugar vijana wa turiani magoli 2-1.Kwa sasa Simba ina point 59 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi point ambazo hakuna timu itakayoweza kuzifikia hata ikishinda magoli 100 katika mchezo unaofuata, Azam anaifuatia simba katika msimamo huku akiwa na point 53 na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Kagera sugar mchezo ambao hata akishinda hauwezi kubadili msimamo wa ligi kwani itakuwa na jumla ya point 56 pungufu ya zile za Simba ambayo ina 59.



2.LA LIGA (HISPANIA)
-Ushindi wa jana wa Real madrid umewapa ubingwa na kumaliza miaka minne ya utawala wa Barcelona


Madrid wakishangila ubingwa wa La liga baada ya ushindi wao wa mabao matatu dhidi ya Athletic Bilbao

 3.FRANCE- LIGUE 1
-Mpambano mkali upo dhidi ya timu tatu huku Montpellier ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa endapo itashinda mechi zake zote.

 1.  Montpellier 35 22 7 6 63 33 73

 2.  PSG 35 20 10 5 66 37 70



 3.  Lille 35 19 11 5 65 37 68



4. ENGLAND- PREMIIERSHIP
- Timu mbili toka jiji la Manchester ndiyo pekee zenye nafasi ya kutwaa ubingwa huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa bingwa kupatikana kwa kuzingatia uwiano wa magoli endapo timu hizi zitashinda mechi zote zilizobaki.





GP W D L GS GA P


 1.  Manchester City 36 26 5 5 88 27 83

 2.  Manchester United 36 26 5 5 86 33 83





























ry








No comments:

Post a Comment