SIMBA, MORO UNITED KUCHEZA USIKU
Mechi ya Ligi ya Vodacom kati ya Simba
na Moro United iliyokuwa ichezwe Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imerudishwa nyuma hadi Jumatatu ya Aprili 23 mwaka
huu kwenye uwanja huo huo na itaanza saa 1 kamili usiku.
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kuipa
Simba fursa ya kujiandaa vizuri kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho la
Afrika dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Pia mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar
iliyokuwa ichezwe Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es
Salaam imesogezwa mbele hadi Aprili 22 mwaka huu kupisha mechi ya U20
kati ya Tanzania na Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine mbili zimefanyiwa
marekebisho; Coastal Union na Kagera Sugar zilizokuwa zicheze jijini
Tanga, Aprili 29 mwaka huu, mechi yao imesogezwa hadi Aprili 30 mwaka
huu ili kupisha shughuli za Mei Mosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Nazo
Azam na Toto Africans zilizokuwa zicheze Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa
Chamazi, sasa zitacheza Aprili 28 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:
Post a Comment