MAHAKAMA YATENGUA MATOKEO YA UBUNGE SUMBAWANGA MJINI
Ushindi alioupata mgombea wa CCM ndugu Hilal Aeshy jimbo la Sumbawanga mjini katika uchaguzi wa 2010 yametenguliwa leo na mahakama baada ya jaji kijiridhisha na hoja zilizotolewa na upande wa mashitaka (Ndugu Norbert Yamsebo wa CHADEMA) kuwa ndugu Aeshi alipata ushindi kwa kutumia rushwa
Pichani Mwl. Norbert Yamsebo.
Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu
wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea
vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa
kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa
mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo,
mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi
kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.
Moja ya kituko kilichotokea katika kesi hii mara baada ya mbunge huyo kuulizwa kama
anaamini kuwa alishinda uchaguzi na kusema hajui kama alishinda ila mkurugenzi ndiye anayejua
ushindi huo.
Umati ulijitokeza kwa wingi sana na watu walijaa ndani hivyo ilibidi
spika zifungwe nje na mara baada ya hukumu kusomwa wafuasi wa CHADEMA walionekana wakishangilia kwa furaha.

No comments:
Post a Comment