KAMATI YA TIBAIGANA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA YANGA.
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeitupili mbali rufaa ya Yanga, kupinga kopokonywa pointi tatu ilizozivuna kwenye mechi na Coastal Union ya Tanga.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wake, Alfred Tibaigana, kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam zimesema rufaa ya Yanga imetupwa.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wake, Alfred Tibaigana, kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam zimesema rufaa ya Yanga imetupwa.
Yanga
iliifunga Coastal 1-0, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la
Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza, lakini Kamati ya Ligi Kuu
ikawapokonya pointi kwa kosa la kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’
aliyekuwa anatumikia adhabu.
Kupokwa
pointi hizo, kunamaanisha Yanga sasa iko hatarini kukosa nafasi ya
kucheza michuano ya Afrika mwakani, kutokana na Simba SC sasa kuwa
inaongoza ligi kwa pointi zake 53 na Azam yenye pointi 50 inashika
nafasi ya pili.
Yanga yenye pointi 43 inashika nafasi ya tatu na leo itakuwa mgeni wa Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.

No comments:
Post a Comment