MAHAKAMA YATENGUA MATOKEO YA UBUNGE SUMBAWANGA MJINI
Ushindi alioupata mgombea wa CCM ndugu Hilal Aeshy jimbo la Sumbawanga mjini katika uchaguzi wa 2010 yametenguliwa leo na mahakama baada ya jaji kijiridhisha na hoja zilizotolewa na upande wa mashitaka (Ndugu Norbert Yamsebo wa CHADEMA) kuwa ndugu Aeshi alipata ushindi kwa kutumia rushwa
Pichani Mwl. Norbert Yamsebo.
Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu
wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea
vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa
kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa
mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo,
mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi
kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.
Moja ya kituko kilichotokea katika kesi hii mara baada ya mbunge huyo kuulizwa kama
anaamini kuwa alishinda uchaguzi na kusema hajui kama alishinda ila mkurugenzi ndiye anayejua
ushindi huo.
Umati ulijitokeza kwa wingi sana na watu walijaa ndani hivyo ilibidi
spika zifungwe nje na mara baada ya hukumu kusomwa wafuasi wa CHADEMA walionekana wakishangilia kwa furaha.
Monday, April 30, 2012
SIMBA KUIPA NAFASI YANGA MICHUANO YA AFRICA MWAKANI
Hiyo ni kwa mujibu wa kanuni mpya za mashindano ya klabu Afrika za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwamba nchi ambazo kwa sasa zina nafasi moja moja za kuingiza timu kwenye michuano ya klabu, zitakuwa zikiongezewa nafasi moja moja katika michuano ambayo klabu yake imefanikiwa kuingia hatua ya makundi.
Kwa mfano mwaka huu Sudan imeshirikisha timu nne kwenye michuano hiyo, mbili Ligi ya Mabingwa na mbili Kombe la Shirikisho, kwa sababu msimu uliopita iliingiza timu zake kwenye hatua za makundi za michuano yote hiyo.
Tanzania bado ina nafasi moja moja tu ambazo hadi sasa tayari Simba na Azam zimejihakikishia kucheza kwa msimu ujao.
Jioni ya jana, Simba SC imeonyesha dalili za kuifungulia njia Tanzania kuingiza timu tatu kwenye michuano ya Afrika mwakani, moja Ligi ya Mabingwa na mbili Shirikisho, baada ya kujiwekea mazingira mazuri ya kuingia kwenye hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho kwa kuifunga Al Ahly Shandy mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sasa Simba inahitaji sare yoyote au kufungwa si chini ya mabao 2-0, ili kuuungana na timu nane zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho.
Maana yake- Simba ikiitoa Al Ahly Shandy itacheza na timu iliyotolewa Ligi ya Mabingwa ili kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi.
Simba jana ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi wa mabao 5-0, kama si kupoteza penalti kipindi cha kwanza na nafasi moja ya wazi mnamo kipindi cha pili.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo, kilikuwa kigumu kwa Simba, lakini baada ya kupata mawaidha ya kocha wao, Profesa Milovan Cirkovic, Simba waliingia na mvua ya mabao kipindi cha pili na kuufanya Uwanja wenye uwezo wa kumeza mashabiki 60,000 uchangamke.
Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’, dakika ya 66 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Felix Mumba Sunzu Jr. Sunzu alipokea pasi ndefu ya Uhuru Suleiman Mwambungu, ambaye aliuwahi mpira uliookolewa baada ya Simba kushambuliwa.
Sunzu alifanya kazi nzuri ya kumtoka beki wa Shandy, Fareed Mohamed kabla ya kumpa pasi mfungaji.
Bao la pili la Simba lilifungwa na Patrick Mutesa Mafisango, baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Emmanuel Arnold Okwi kuwatoka mabeki wa Shandy.
Bao la tatu la Simba lilipatikana dakika ya 86, mfungaji Emanuel Okwi kufuatia gonga safi ya wachezaji wa Simba kwenye eneo la hatari la Shandy.
Boban alikaribia kufunga tena kabla ya hapo, baada ya kupewa pasi nzuri akiwa amebaki yeye na kipa, lakini akapiga juu ya lango.
Source: Abdallah Sulay
Imewekwa na Hillary E. Sandagila
Friday, April 27, 2012
Baraza la Mawaziri la Tanzania kuvunjwa
Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo.;
A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;
Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.
1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri
B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.
Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.
Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.
Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary
BREAKING NEWS:- TUNDU LISSU ASHINDA KESI YA KUPINGA UBUNGE WAKE
- Hoja zote za upande wa mlalamikaji zatupwa.
- Maofisa Jeshi pamoja na kikosi maalum waudhulia maakamani.
Mbunge
wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, ameshinda kesi
iliyofunguliwa dhidi yake mjini Singida kupinga ushindi uliomweka
madarakani
Hukumu
imetolewa na Jaji Moses Mzuna anayetoka mahakama kuu kanda ya
Kilimanjaro, iliyofunguliwa na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na
Pascal Hallu.
Kesi
hiyo imekuwa kivutio sana kwa wananchi wengi wa mkoa Singida na nchini
kwa ujumla, kutokana na umaarufu wa mbunge huyo machachari.
Leo
mahakamani wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida,
na waandishi wa habari walijitokeza kwa wingi sana katika eneo la
mahakama.
Idadi
ya Polisi pia ilikuwa kubwa, ndani na nje ya mahakama.Kilicho kuwa cha
ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa jeshi la polisi
walikuwepo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kukagua kila anayeingia
mahakamani, kila mtu aliyekuwa anaingia mahakamani alipekuliwa hadi
wabunge waliokuja kusikiliza kesi hiyo.
Akisoma
hukumu Jaji Moses Mzuna alisema “HOJA YA TISA, Kama Mgombea wa
walalamikaji (CCM) alikataa kusaini matokeo. Hoja hii haipaswi
kunipotezea muda sana. Njau hakuhudhuria, aliwakilishwa na mlalamikaji
wa kwanza ambaye alikataa kusaini matokeo.
Wakili
wa serikali alisema, kukataa pekee kusaini matokeo hakusaidii kutengua
matokeo. Hivyo hata hoja ya tisa naitupilia mbali. Haikuwa sahihi.
Hoja
ilitolewa hapa, kuwa mawakala walikula kiapo kwa hakimu. Walalamikaji
walisema kuwa walipaswa kula kiapo kwa msimamizi wa uchaguzi. Je
kuapishwa na hakimu kunabatilisha matokeo?
Hoja
zilizotolewa na mawakili wa serikali walisema Hakimu ana mamlaka ya
kutoa viapo. Binafsi nasema kuwa waliotunga sheria hawakumaanisha kuwa
Mahakimu hawaruhusiwi kuapisha mawakala, vinginevyo kungekuwepo fomu ya
hakimu tu. Lakini fomu zinaonyesha hakimu, Msimamizi wa uchaguzi na
Msimamizi msaidizi, fomu inatambulika kisheria, kwa sheria ya Uchaguzi.
Hii haihusiani na zoezi la uchaguzi.
Katika kesi ya Prince bagenda Vs Wilson masilingi, katika kesi hii
mawakala walifanya kazi bila kuapishwa, na ilichukuliwa kuwa sehemu ya kutengua uchaguzi, angalia pg 240.
mawakala walifanya kazi bila kuapishwa, na ilichukuliwa kuwa sehemu ya kutengua uchaguzi, angalia pg 240.
Kwa
lugha yake jaji alisema hawakuwa na mamlaka halali, lawful mandate,
lakini ilisaidia kutengua, na mwanasheria wa serikali alihusika katika
hili.
Maelezo
hayo yanatofautiana na kesi iliyo mbele yangu, jimbo la Singida
mashariki mawakala walikula kiapo, na walikuwa na mamlaka halali. Hivyo
hoja hii naitupilia mbali
HIVYO, UCHAGUZI ULIKUWA WA HAKI, NA TUNDU LISSU NI MBUNGE HALALI NA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA WA HAKI, HIVYO SIWEZI KUTENGUA.
Walalamikaji
wa kesi hiyo, iliyofunguliwa mahakama kuu kanda ya Dodoma, walikuwa
wanatetewa na wakili Godfrey Wasonga, kutoka mkoani Dodoma, huku Lissu
akijisimamia mwenyewe.
Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012, kufuatia makada wawili wa CCM,
kupinga ushindi wa Lissu kwa madai kuwa uchaguzi huo uligubikwa
na dosari nyingi.
Awali
Katika mahojiano na Lissu, alisema vyovyote mahakama itakavyo
hukumu, anajivunia kuimarisha demokrasia na kuwa mbunge wa kwanza
kutoka upinzani, kwenye historia ya mikoa ya kanda ya kati.
Thursday, April 26, 2012
TFF YAIPA AZAM POINT 3 NA MAGOLI 3-0 DHIDI YA MTIBWA SUGAR
Release No. 064
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 26, 2012
MECHI YA TWIGA STARS, ZIMBABWE YAFUTWA
Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya
timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) na Zimbabwe iliyokuwa ichezwe
keshokutwa (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imefutwa.
Uamuzi huo umefanywa na Chama cha Mpira
wa Miguu Zimbabwe (ZIFA) ambayo sasa imeamua kucheza mechi ya kirafiki
na Zambia. Mechi hiyo itachezwa Aprili 28 mwaka huu jijini Harare.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi chini
ya kocha wake Charles Boniface Mkwasa katika kambi ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) iliyoko Ruvu mkoani Pwani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linaendelea na jitihada za kuitafutia mechi za kirafiki Twiga
Stars kabla ya kucheza mechi ya mashindano dhidi ya Ethiopia ambayo
itafanyika Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa.
MTIBWA SUGAR YAPOTEZA MECHI DHIDI YA AZAM
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) imemuondoa mwamuzi Rashid Msangi wa Dodoma kwenye
orodha ya waamuzi kwa kuvuruga mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam
na Mtibwa Sugar iliyochezwa Aprili 23 mwaka huu.
Pia waliokuwa waamuzi wasaidizi wa mechi
hiyo; Samuel Mpenzu na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha nao
wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Vilevile Kamati imeipa Azam ushindi wa
mabao 3-0 kwa mujibu wa Ibara ya 31 ya Kanuni za Nidhamu za Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Kwa mujibu wa kanuni hiyo, timu
itakayohesabika kupoteza mechi (Mtibwa Sugar) itakuwa imefungwa mabao
3-0.
Kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi Kuu ya
Vodacom kifungu cha 22(3-6) Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000,
imepoteza mapato yote ya mchezo huo na inatakiwa kulipa faini hiyo kabla
ya mechi inayofuata.
Nao makamishna watatu; Abdallah Mitole
wa Dar es Salaam, William Chibura (Musoma) na Omari Mawela (Mwanza)
wameondolewa kwenye orodha ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushindwa kufika
kwenye mechi walizopangiwa kusimamia bila taarifa.
Makamishna hao wametakiwa kutoa maelezo
ya maandishi wakieleza sababu za kutofika kwenye mechi. Mechi walizokuwa
wamepangia ni Coastal Union vs Ruvu Shooting (Mitole), Kagera Sugar vs
Yanga (Chibura) na Kagera Sugar vs African Lyon (Mawela).
Nayo Moro United imepigwa faini ya sh.
500,000 baada ya wachezaji wake kugoma kuingia kwenye vyumba vya
kubadirishia (dressing rooms) wakati wa mechi namba 171 kati yao na
Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Adhabu hiyo ni kwa
mujibu wa kanuni ya 8(16).
Pingamizi la Villa Squad dhidi ya
African Lyon kuwa wakati wa mechi yao ilitumia wachezaji wawili (Mohamed
Samata na Benedict Jacob) ambao mikataba yao imemalizika limetupwa kwa
vile wana leseni halali za kucheza ligi.
Pia mwamuzi wa mechi namba 160 kati ya
Moro United na Oljoro JKT, Nathaniel Lazaro wa Kilimanjaro amefungiwa
miezi sita na kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa kutozingatia
kutunza muda kwa mujibu wa kanuni ya 26(1)(f).
Vilevile Kamishna wa mechi ya Moro
United na Oljoro JKT, Ali Mkomwa wa Pwani na Said Mnonga wa Mtwara
aliyekuwa mwamuzi msaidizi mechi kati ya Villa Squad na Coastal Union
wameandikiwa barua za onyo wakitakiwa kuwa makini kwenye michezo
wanayosimamia.
9 POLISI WAPIGWA FAINI MIL 1/- KILA MMOJA
Kamati ya Ligi ya TFF imewafungia mechi
tatu na kuwapiga faini y ash. milioni mmoja kila mmoja wachezaji tisa wa
timu ya Polisi Dodoma baada ya kumpiga mwamuzi Martin Saanya kwenye
mechi dhidi ya Azam iliyochezwa Aprili 14 mwaka huu mjini Dodoma.
Wachezaji hao walioadhibiwa kwa mujibu
wa kanuni ya 25(g)(iii) ni Noel Msekwa, Frank Sindato, Abdallah Matila,
Bantu Admin, Salmin Kisi, Madope Mwingira, Sihaba Mkude, Kaliyasa
Mashaka na Ibrahim Massawe.
Iwapo wachezaji hao watahama Polisi na kujiunga na timu nyingine, watahama na adhabu zao.
Vilevile timu ya Polisi Dodoma imepigwa
faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake katika mechi
hiyo iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri. Pia timu hiyo imepewa barua ya onyo
kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi yao na Yanga
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Wednesday, April 25, 2012
MECHI YA SIMBA NA WASUDANI MAANDALIZI YAKAMILIKA.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
NDUGU waandishi.
Kama mnavyofahamu, Jumapili
ya Aprili 29 mwaka huu, timu ya soka ya Simba inakutana na klabu ya Al Ahly
Shandy kutoka Sudan katika
mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ni timu pekee kutoka
katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyobaki katika michuano yote
ya kimataifa inayosimamiwa na CAF.
Kubwa zaidi, ndiyo
wawakilishi pekee wa Tanzania
waliobaki katika michuano ya kimataifa na hivyo wanabeba bendera ya taifa
kokote kule waliko.
Maandalizi yote kwa ajili ya
pambano hilo
yamekamilika.
Wapinzani wetu, Al Ahly
wanatarajiwa kuwasili kesho saa saba mchana kwa ndege ya Ethiopia Airlines.
Waamuzi na Kamishina wa
mchezo wamepangwa kuwasili Ijumaa (keshokutwa) wakitokea nchini Swaziland na Rwanda.
VIINGILIO
Kutokana na ukweli kwamba
mechi hiyo itakuwa ya kimataifa, Simba imepanga viingilio ambavyo kila
mwananchi ataweza kuvimudu. Viingilio vitakuwa kama
ifuatavyo.
Viti vya bluu na kijani
itakuwa Sh. 5,000, Rangi ya Chungwa Sh, 10,000, VIP C 15,000, VIP B 20,000 na VIP
A 30,000.
Tiketi zitauzwa katika maeneo
yafuatayo, Big Bon, Benjamin Mkapa, Stears Mjini, Mbagala Dar Live, OilCom
Buguruni, Tandika Mwembeyanga, Ubungo Oilcom, Mwenge Bus Stand, BP Mwananyamala
na Gapco Ukonga.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku
ya Ijumaa asubuhi katika maeneo yaliyotajwa.
Klabu imepokea maombi mengi
kutoka kwa wanachama na wapenzi wake kutoka mikoani na ingeomba kwamba wale
wanaotaka kuja kutazama mechi hii kwa makundi kutoka mikoani, wawasiliane
mapema na uongozi ili wanunuliwe tiketi zao mapema.
Simba SC imechapa tiketi
za kutosha na ingeomba wapenzi na wanachama wake kujitokeza kwa wingi kwenye
pambano hilo.
Wana Simba wote wanaombwa
kuja uwanjani wakiwa wamevalia mavazi yao
ya rangi Nyekundu na Nyeupe ili uwanja mzima upendeze kwa rangi hizo.
Tunatoa wito kwa vyombo vya
habari kuisaidia Simba na Tanzania
kwa kuelekeza nguvu zao katika uandishi wa taarifa ambazo zitaisaidia timu yetu
kusonga mbele na si kuondoa morali au kusababisha watu wasiende uwanjani.
Shukrani.
Uongozi wa Simba SC
unatoa shukrani, kwa namna ya kipekee kabisa, kwa serikali kutokana na uamuzi
wake wa kuruhusu Wekundu wa Msimbazi kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa
kujiandaa na mechi hii muhimu.
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba
SC
Sunday, April 22, 2012
MANCHESTER UNITED WAENDELEA KUONGOZA KWA UTAJIRI DUNIANI KWA MWAKA WA 8 MFULULIZO - YAZIFUNIKA REAL NA BARCA.
Manchester United wametajwa tena kama timu ya soka tajiri zaidi duniani - wakitajwa kuwana thamani ya £1.39billion.
Mabingwa hao wa Uingereza wamekaa
kileleni mwa listi ya jarida la kimarekani la Forbes kwa miaka 8
mfululizo kufuatia mwaka mwingine wa mafanikio chini ya Sir Alex
Ferguson.
Majirani zao Manchester City wenyewe pamoja na matanuzi yote ya Fedha hawajaweza hata kuingia Top 10 - wakishika nafasi ya 13.
Timu nyingine ya kiingereza
iliyofuata nyayo za United ni Arsenal waliopo nafasi ya nne, wakifuatiwa
na Chelsea katika nafasi ya saba, Liverpool wapo nafasi ya 8 na
Tottenham wakiwa nafasi ya 11.
Giants wa Spain Real Madrid wapo
nafasi ya pili, wakifuatiwa na wapinzani wao Barcelona. Bayern Munich
wamekamta nafasi ya tano.
LISTI KAMILI TIMU TAJIRI DUNIANI BY FORBES MAGAZINE
| Rank | Team | Current Value ($mil) | 1-Yr Value Change (%) | Debt/Value (%) | Revenue ($mil) | Operating Income ($mil) |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Manchester United | 2,235 | 20 | 32 | 532 | 178 |
| 2 | Real Madrid | 1,877 | 29 | 13 | 695 | 214 |
| 3 | Barcelona | 1,307 | 34 | 54 | 653 | 96 |
| 4 | Arsenal | 1,292 | 8 | 32 | 364 | 98 |
| 5 | Bayern Munich | 1,235 | 18 | 13 | 466 | 90 |
| 6 | AC Milan | 989 | 18 | 9 | 341 | 29 |
| 7 | Chelsea | 761 | 16 | 22 | 362 | 76 |
| 8 | Liverpool | 619 | 12 | 8 | 295 | 45 |
| 9 | Juventus | 591 | -8 | 15 | 223 | -38 |
| 10 | Schalke 04 | 587 | 56 | 40 | 293 | 101 |
ORODHA YA WABUNGE WALIO TIA SAINI
1. Rashid Ali Abdallah – CUF
2. Chiku Aflah Abwao- Chadema
3. Saluim Ali Mbarouk – CUF
4. Salum Khalfam Barwany – CUF
5. Deo Haule Filikuchombe- CCM
6. Pauline Philipo Gekul- Chadema
7. Asaa Othman Hamad- CUF
8. Prof.Kuliyokela Kahigi- Chadema
9. Naomi Mwakyoma Kaihula – Chadema
10. Sylvester Kasulumbayi- Chadema
11. Raya Ibrahim Khamis - Chadema
12. Mkiwa Hamad Kiwanga - CUF
13. Susan Limbweni Kiwanga- Chadema
14. Grace Sindato Kiwelu –Chadema
15. Kombo Khamis Kombo – cuf
16. Joshua Samwel Nassari – Chadema
17. Tundu Antiphas Lissu- Chadema
18. Aphaxar Kangi Lugola- CCM
19. Susan Anselim Lymo- Chadema
20. Moses Machali – NCCR Mageuzi
21. John Shibuda Magalle – Chadema
22. Faki Haji Makame- CUF
23. Esther Nicholas Matiko- Chadema
24. Joseph Osmund Mbilinyi- Chadema
25. Freman Aikaeli Mbowe- Chadema
26. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – Chadema
27. Halima James Mdee-Chadema
28. John John Mnyika- Chadema
29. Augustino Lyatonga Mrema- TLP
30. Maryam Salum Msabaha- Chadema
31. Peter Msingwa-chadema
32. Christowaja Gerson Mtinda- Chadema
33. Philipa Geofrey Mturano- Chadema
34. Christina Lissu Mughwai- Chadema
35. Joyce John Mukya – Chadema
36. Mchungaji Israel Yohane Natse – Chadema
37. Philemon Ndesamburo- Chadema
38. Ahmed Juma Ngwali- CUF
39. Vincent Josephat Nyerere- Chadema
40. Rashid Ali Omar- CUF
41. Meshack Jeremiah Opulukwa- Chadema
42. Lucy Philemon Owenya- Chadema
43. Rachel Mashishanga- Chadema
44. Mhonga Said Ruhwanya – Chadema
45. Conchesta Rwamlaza – Chadema
46. Moza Abedi Saidy- CUF
47. Joseph Roman Selasini – Chadema
48. David Ernest Silinde- Chadema
49. Rose Kamili Sukum - Chadema
50. Cecilia Daniel Paresso- chadema
51. Kabwe Zuberi Zitto- Kigoma Kaskazini
52. Magdalena Sakaya – CUF
53. Rebecca Mngodo- CUF
54. Sabreena Sungura -Chadema
55. Hamad Rashid Mohammed- CUF
56. Rukia Kassim Ahmed- CUF
57. Mustapha Boay Akoonay -Chadema
58. Abdalla Haji Ali -CUF
59. Khatibu Said Ali -CUF
60. Hamad Ali Hamad -CUF
61. Riziki Omar Juma -CUF
62. Haji Khatibu Kai -CUF
63. Anna Marystella John Malack -Chadema
64. Hamad Rashid Mohamed -CUF
65. Rajab Mbarouk Mohamed -CUF
66. Thuwayba Idrissa Muhamed -CUF
67. Masoud Abdallah Salum -CUF
68. Muhamad Ibrahim Sanya -CUF
69. Ali Khamis Seif -CUF
70. Haroub Muhammed Shamis -CUF
71. Amina Amour Nassoro -CUF
Thursday, April 19, 2012
SIMBA, MORO UNITED KUCHEZA USIKU
Mechi ya Ligi ya Vodacom kati ya Simba
na Moro United iliyokuwa ichezwe Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imerudishwa nyuma hadi Jumatatu ya Aprili 23 mwaka
huu kwenye uwanja huo huo na itaanza saa 1 kamili usiku.
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kuipa
Simba fursa ya kujiandaa vizuri kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho la
Afrika dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Pia mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar
iliyokuwa ichezwe Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es
Salaam imesogezwa mbele hadi Aprili 22 mwaka huu kupisha mechi ya U20
kati ya Tanzania na Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine mbili zimefanyiwa
marekebisho; Coastal Union na Kagera Sugar zilizokuwa zicheze jijini
Tanga, Aprili 29 mwaka huu, mechi yao imesogezwa hadi Aprili 30 mwaka
huu ili kupisha shughuli za Mei Mosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Nazo
Azam na Toto Africans zilizokuwa zicheze Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa
Chamazi, sasa zitacheza Aprili 28 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Wednesday, April 18, 2012
KAMATI YA TIBAIGANA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA YANGA.
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeitupili mbali rufaa ya Yanga, kupinga kopokonywa pointi tatu ilizozivuna kwenye mechi na Coastal Union ya Tanga.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wake, Alfred Tibaigana, kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam zimesema rufaa ya Yanga imetupwa.
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana chini ya Mwenyekiti wake, Alfred Tibaigana, kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam zimesema rufaa ya Yanga imetupwa.
Yanga
iliifunga Coastal 1-0, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la
Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza, lakini Kamati ya Ligi Kuu
ikawapokonya pointi kwa kosa la kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’
aliyekuwa anatumikia adhabu.
Kupokwa
pointi hizo, kunamaanisha Yanga sasa iko hatarini kukosa nafasi ya
kucheza michuano ya Afrika mwakani, kutokana na Simba SC sasa kuwa
inaongoza ligi kwa pointi zake 53 na Azam yenye pointi 50 inashika
nafasi ya pili.
Yanga yenye pointi 43 inashika nafasi ya tatu na leo itakuwa mgeni wa Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
Monday, April 16, 2012
Prof.BAREGU aeleza kwa nini hakutumia Biblia kuapa
"I was baptized a Catholic when i was young at school..i wouldnt want to be hyprocrite as i believe God is there(is sovereign and exists), not in the house of bibles or Qurans..i ve never been doctrinaire for Christianity or any religion from abroad, i believe in a lot of things in Africa..Africans ve abondoned their indigenous spiritualism from their own 'Gods' and what they do now is nothing other than hyprocricy..
There is spiritual push from the devevoloped world but still some respect their denominations.For example, Hinduism is still playing a big role and most respected by Indians communities."
Baregu subsribes to humanity,justice,equality ,clean environment, fairness and equity,between community and conscious building.
Source:The African,Monday,April 16 2012.
ARUSHA WASEMA MUNGU ANAJIBU MAOMBI PAPO KWA PAPO!!
BAADA YA MFUNGO WA SIKU SABA AMBAO LEO NDIO KILELE,MUNGU ATUPA ISHARA YUPO PAMOJA NASI.....
Yani walichokifanaya mahakama na ccm kwa mbunge wetu Godbless Lema ni
jambo ambalo naamini kwa maombi yale tuliyoyaanza toka jumanne ilopita
ule mfungo wetu Mungu ameusikia na leo ndio pigo la kwanza kwa
UVCCM,Sasa hiyo ni trela tu,bado tutegemee mpasuko mkubwa ndani ya
ccm.......Mungu wetu huwa anatusikiliza sana kwa maana anajua tuko
pamoja nae.......
Sunday, April 15, 2012
VPL YAFIKIA PATAMU
Mafisango aiweka pazuri Simba, Toto waikamata Yanga
Goli la kiungo toka nchini Rwanda Patrick Mafisango lilitosha kuwapa point 3 Simba SC, wakati mpinzani wake wa jadi Yanga akilala goli 3 toka kwa Toto Africa katika muendelezo wa michezo ligi kuu ya vodacom.
SIMBA YAJIKITA KILELENI
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba SC wameendelea kukalia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom, baada ya kuwachapa Ruvu Shooting goli 1-0 katika nyasi za uwanja wa Taifa na kufanya wigo wa point baina yake na Azam kuwa 3.
Simba ilibidi wangoje mpaka dakika ya 80 ndipo walipo pata goli lao la ushindi lililofungwa na Patrick Mutesa Mafisango.
TOTO AFRICA WAITOA RELINI YANGA
Kwa mara ya kwanza katika historia ya uwanja wa CCM Kirumba kushuhudia Toto Africa akiibuka na ushindi mbele ya Yanga iliyo katika mbio za kusaka ubingwa wa Tanzania Bara.
Katika mchezo huo Toto Africa waliwaduwaza Yanga baada ya kupata goli katika dakika ya 18 kupitia kwa Mussa Said na Kabla hawajakaa sawa walishangaa wanafungwa la pili kupitia kwa Kulwa Mobbi katika dakika ya 24.
Mussa Saidi alirejea kwenye nyavu za yanga katika dakika ya 39, huku yanga walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Hamisi kiiza dakika ya 43. Na Toto kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3-1.
Yanga walirejea kipindi cha pili na kupata goli la pili kupitia kwa Hamisi Kiiza katika dakika ya 65, likiwa ni goli lake la pili katika mchezo wa leo na kupelekea mchezo kumalizika kwa Yanga kufungwa goli 3-2 na Toto Africa.
Kocha mkuu wa Yanga Mserbia, Kosradin Papic alizomewa na mashabiki wa Yanga mjini Mwanza kutokana na kiwango kibovu ambacho timu hiyo inacheza hivi sasa.
Kwa matokeo hayo yanapelekea kutofautiana kwa point 10 na vinara Simba na point 7 kutoka kwa Azam lakini wakiwa nyuma mchezo mmoja.
MCHEZO MWINGINE
COASTAL UNION 2-4 VILLA SQUAD
Saturday, April 14, 2012
MAN CITY YAIONGEZEA PRESSURE MAN UNITED
Norwich City vs Manchester City Report
Adam Johnson
90+3
Norwich City vs Manchester City Report
| 4/14/12 Live | 7:30 AM EDT | Norwich City vs. Manchester City (Live Only) |
Played
April 14, 2012 7:45 AM EDT
Carrow Road — Norwich, Norfolk
Referee: C. Foy
Attendance: 26812
April 14, 2012 7:45 AM EDT
Carrow Road — Norwich, Norfolk
Referee: C. Foy
Attendance: 26812
51′
Andrew Surman
TIMU ZA MAJESHI ZAENDELEA KUCHUANA KUINGIA LIGI KUU
Msimamo wa Ligi
MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM (VPL)
| Rank | Team | GP | W | D | L | GD | Pts |
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Simba SC | 22 | 15 | 5 | 2 | 23 | 50 |
| 2 | Azam FC | 22 | 14 | 5 | 3 | 22 | 47 |
| 3 | Yanga SC | 21 | 13 | 4 | 4 | 13 | 43 |
| 4 | Mtibwa Sugar | 22 | 10 | 4 | 8 | 7 | 34 |
| 5 | Coastal Union | 22 | 10 | 2 | 10 | -1 | 32 |
| 6 | JKT Ruvu | 22 | 7 | 9 | 6 | -2 | 30 |
| 7 | JKT Oljoro | 22 | 7 | 7 | 8 | -4 | 28 |
| 8 | Ruvu Shooting | 22 | 6 | 9 | 7 | 1 | 27 |
| 9 | Kagera Sugar | 21 | 5 | 9 | 7 | -2 | 24 |
| 10 | African Lyon | 21 | 5 | 6 | 10 | -6 | 21 |
| 11 | Toto African | 21 | 3 | 11 | 7 | -7 | 20 |
| 12 | Villa Squad | 22 | 5 | 4 | 13 | -19 | 19 |
| 13 | Moro United | 22 | 3 | 9 | 10 | -13 | 18 |
| 14 | Polisi Dodoma | 22 | 3 | 8 | 11 | -12 | 17 |
MSIMAMO WA LIGI DARAJA LA KWANZA 9 BORA
| Rn | Team | GP | W | D | L | GD | Pts |
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Mgambo Shooting | 5 | 3 | 2 | 0 | 6 | 11 |
| 2 | Polisi Moro | 4 | 3 | 1 | 0 | 7 | 10 |
| 3 | T. Prisons | 4 | 2 | 1 | 1 | 1 | 7 |
| 4 | Polisi DSM | 5 | 1 | 3 | 1 | 2 | 6 |
| 5 | Mbeya City | 4 | 1 | 2 | 1 | 1 | 5 |
| 6 | Rhino Ranger | 5 | 1 | 2 | 2 | -2 | 5 |
| 7 | Polisi Tabora | 4 | 1 | 1 | 2 | -3 | 4 |
| 8 | Mlale | 4 | 1 | 1 | 2 | -5 | 4 |
| 9 | Trans Camp | 5 | 0 | 1 | 4 | -7 | 1 |
UKATAE UKUBALI SIMBA NDO BABA YAO AFRIKA MASHARIKI NA KATI
SASA ni rasmi kwamba Simba SC ndiyo fahari ya nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Simba ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki ambayo imebaki katika michuano ya makombe yanayosimamiwa na Shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, hakuna timu kutoka katika jumuiya hiyo ambayo bado ipo katika michuano hiyo ukiondoa Simba SC. Nchi tano zinaunda Jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Orodha hiyo inaonyesha kwamba nchi ya Sudan ndiyo kinara kwa ngazi ya vilabu barani Afrika kufikia sasa baada ya kuingiza timu nne katika michuano ya Ligi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la CAF.
Timu ambazo Sudan imeingiza katika michuano hiyo ni El Merreikh na Al Hilal ambazo zimesonga mbele katika Ligi ya Mabingwa na Al Ahly Shandy na El Amal ambazo zimesonga mbele katika Kombe la Shirikisho (CAF).
Shandy ndiyo timu ambayo itacheza na Simba katika hatua ya 16 bora baadaye mwezi huu.
Simba tunu ya Afrika Mashariki
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Simba ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki ambayo imebaki katika michuano ya makombe yanayosimamiwa na Shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, hakuna timu kutoka katika jumuiya hiyo ambayo bado ipo katika michuano hiyo ukiondoa Simba SC. Nchi tano zinaunda Jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Orodha hiyo inaonyesha kwamba nchi ya Sudan ndiyo kinara kwa ngazi ya vilabu barani Afrika kufikia sasa baada ya kuingiza timu nne katika michuano ya Ligi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la CAF.
Timu ambazo Sudan imeingiza katika michuano hiyo ni El Merreikh na Al Hilal ambazo zimesonga mbele katika Ligi ya Mabingwa na Al Ahly Shandy na El Amal ambazo zimesonga mbele katika Kombe la Shirikisho (CAF).
Shandy ndiyo timu ambayo itacheza na Simba katika hatua ya 16 bora baadaye mwezi huu.
Friday, April 13, 2012
Friday, April 13, 2012
Fabrice Muamba awapatia keki wafanyakazi wa hospital.
Kiungo wa Bolton Wonderers Fabrice Muamba muda wowote kutoka hivi sasa sasa anaweza kutoka Hospitalini baada ya afya yake kutengamaa
NAFASI ZA AJIRA MKOANI RUVUMA ZATANGAZWA
Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa
kushirikiana na wafadhili Walter Reed, wanatangaza nafasi za kazi kama
ifuatavyo:-
1.
PROGRAMME OFFICER:NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
•
Kusimamia
na kuratibu shughuli za mpango wa Huduma kwa wanaoishi na Virusi vya
UKIMWI kwa kushirikiana na Mratibu wa Kudhibiti maambukizi ya UKIMWI
Mkoa (Tiba)
•
Kutekeleza kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Msimamizi wa Huduma za Afya Mkoa
Sifa za kuingilia:
-
Wenye shahada ya Udaktari (MD) au Stashahada ya Udaktari (AMO) ambaye amehitimu katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
-
Asiwe mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine ya Serikali na Serikali za Mitaa ndani ya Mkoa.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
2.
AFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI (MONITORING & EVALUATION OFFICER 1 NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
•
Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya mradi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
•
Kuwezesha
na kutoa ushauri na tafsiri ya Sera, Mipango, mikakati na miongozo
kuhusu taarifa za Afya kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Afya
•
Kutekeleza kazi nyingine kama zitakavyoelekezwa na Meneja wa Mradi
Sifa za kuingilia:
-
Wenye Shahada/Shahada ya Uzamili katika fani ya Mipango, Uchumi na Takwimu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
-
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
3.
MHASIBU:
Kazi za kufanya:
•
Kufanya kazi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
•
Kusimamia shughuli zote za Uhasibu katika Mradi
•
Kudhibiti hati za malipo
•
Kujibu hoja za Ukaguzi
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
SIFA ZA KUINGILIA:
-
Awe na Shahada au Stashahada ya Uhasibu kutoka kwenye vyuovinavyotambuliwa na Serikali
4.
WATUNZA KUMBUKUMBU NAFASI TANO (5)
Kazi za kufanya:
•
Kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Meneja wa Mradi
•
Kuandaa na kutunza taarifa /kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Mradi
•
Kukusanya na kuhifadhi taarifa mbalimbali za wagonjwa.
Sifa za kuingilia:
-
Awe na Shahada au Stashahada, au cheti cha utunzaji wa kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
Maombi yote yatumwe kwa:
Katibu Tawala wa Mkoa,
S.L.P. 74,
SONGEA.
AU
Mganga Mkuu wa Mkoa,
S.L.P. 5,
SONGEA.
Subscribe to:
Comments (Atom)






















