Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa baada ya uchaguzi kumalizika, mwenyekiti wa tume hiyo Rita Makaru amesema kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na maofisa wa uchaguzi wa tume hiyo, anaamini kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki. Takriban watu milioni 6.4 ambao ni nusu ya idadi ya watu wa Zimbabwe, wamejiandikisha kupiga kura katika vituo zaidi ya elfu 9, ili kumchagua kati ya rais Robert Mugabe na mpinzani wake mkubwa na wa zamani waziri mkuu Morgan Tsvangirai ambao wanawania kiti cha urais.
Wakati huohuo zoezi la kuhesabu kura limeanza na tume imesema matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutolewa baada ya siku tano.
Mtandao huu utakuretea matokeo hayo mara yatakapoanza kutangazwa. STAY TUNED.

No comments:
Post a Comment