Friday, January 17, 2014

CHADEMA USUKA YAHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI MICHEZO



Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Usuka walizitumia sherehe za Krismas na mwaka mpya kuwahamasisha vijana katika kata hiyo kujihusisha na michezo kwani michezo ni afya na ajira pia, Chama hicho kupitia viongozi wa CHADEMA kata ya Usuka waliandaa mchezo wa mpira wa miguu baina ya timu ya Lion ya Iteni na timu ya kata ya Usuka iliyoundwa na wachezaji wa Usuka na Iteni huku vijiji vya Ikwega, Lugoda na Matowo vikishindwa kushiriki kutokana kile kilichoelekezwa kuwa eti kushiriki mchezo ulioandaliwa na CHADEMA ni kukiunga mkono chama hicho jambo ambalo lilipingwa vikali na waandaaji Kupitia mwenyekiti wa CHADEMA kata ndugu J.Sapali.
Katika maadhimisho hayo chama hicho Kiliandaa zawadi kwa Mshindi wa Kwanza Tsh.50,000 na mshindi wa pili Tsh. 40,000 huku mmiliki wa Blog hii akitoa zawadi kwa Mchezaji bara, Golikipa bora na Mchezaji mwenye nidhamu.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika ktk uwanja wa shule ya msingi Usuka tar 25/12/2013 timu ya Kata ya usuka iliibuka na Ushindi wa magoli mawili dhidi ya goli moja la Lion ya Iteni (2-1) na katika mchezo wa marudiano uliochezwa tar. 1/1/2014 timu hizo zilitoka suluhu bila ya kufungana na hivyo Timu ya kata ya Usuka kuibuka mabigwa wa bonaza hilo na kuzawadiwa Tsh. 50,000 na Lion ya Iten ilichukua Tsh 40,000 kama washindi wa pili, ktk zawadi ya uchezaji bora Mchezaji Kamti toka Usuka alipewa zawadi ya mchezaji mwenye nidhamu, Kipa wa Lion Mlyuka aichaguliwa kuwa kipa bora huku P. Mbugi wa Lion akipewa zawadi ya uchezaji bora.
Akizungumza na mashabiki wa kandanda mbele ya mtendaji wa kijiji cha Iteni aliyekuwa mgeni wa heshima wa mchezo huo Bw. Mahashishi ambaye aliongozana na Bw. Mgavilenzi (katibu wa jimbo la Wanging'ombe) aliwataka vijana kushiriki michezo bila kujali imeandaliwa na chama gani kwani nje ya siasa sisi sote ni ndugu.


Pichani ni mmiliki wa blogi hii akifanya akipiga danadana kabla ya mpira kuanza.  
Kulia Kocha wa timu ya kata ya Usuka Ndg. Peter Changila akifuatilia mchezo kwa makini

Mvua iliyonyesha wakati mchezo ukiendelea haikufanya mchezo usimame

Kocha wa Usuka akitoa maelekezo kwa vijana wake wakati wa mapumziko
Baada ya mchezo kumalizika zawadi zilikabidhiwa kwa washindi
Mmiliki wa blog hii anatoa Pongezi kwa waandaaji wa Mchezo huo hususani Ndg. J.Sapali (mwenyekiti), D.Mbiduka (katibu) na L.Kiswaga (mtunza hazina) kwa ubunifu wao nashauri hata vyama vingine viige utaratibu huu na isiwe kwa mpira wa miguu tuu bali na michezo mingine. HERI YA MWAKA MPYA.

1 comment: